SHIVYAWATA imeendelea kuendesha Mafunzo ya Uelewa wa Haki kwenye Uongozi na Ushiriki wa kisiasa kwa Watu wenye Ulemavu
Watu wenye Ulemavu wamepata kuongeza uelewa wao katika kutetea haki zao kwenye uongozi na ushiriki wa kisiasa kufuatia mfululizo wa vikao vya mafunzo kwa watu zaidi ya 300 ambao ni viongozi wa vyama vya watu wenye Ulemavu nchini Tanzania.
Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) limeendesha mafunzo ya uelewa wa haki zao katika Mikoa nane na kuwafikia watu kutoka wilaya 41 na Mikoa miwili Zanzibar mwezi wa Agosti.
Vikao vya mafunzo vilijikita katika masuala ya haki za uongozi na ushiriki wa kisiasa pamoja na wajibu wa Viongozi wa watu wenye ulemavu Viongozi katika Kuhamasisha uongozi na ushiriki wa kisiasa wa watu wenye ulemavu.
Pia mafunzo yalitoa maelezo ya jumla ya mfumo wa uchaguzi nchini Tanzania, mchakato wa uchaguzi na sheria na jukumu la Taasisi muhimu kama vile NEC na ZEC, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na asasi za kiraia katika Uchaguzi. Kufuatia mafunzo hayo Washiriki walisema sasa watahakikisha wanapiga kura kwenye siku ya uchaguzi baada ya kuongezeka uelewa juu ya umuhimu wa kupiga kura.
Mafunzo hayo yaliwawekwa Washiriki katika jukwaa la kubadilishana mawazo na changamoto. Ulinzi na usalama ni moja ya sababu ya kawaida Washiriki kuwazuia kutaka kushiriki katika michakato ya kisiasa, masalani wakati wa mafunzo yaliyofanyika katika Mkoa wa Mara mjini Musoma Washiriki wenye ulemavu wa ngozi walisema hawaoni ni salama kwenda kwenye Mikutano sababu ya hatari ya kutekwa / mauaji kwasababu ya sehemu za miili yao. Hayo yalisemwa na Bi Happiness Manobi ambaye amekuwa akitishiwa kwa SMS Mara kadhaa na alikuwa chini ya ulinzi wa polisi.
Hata hivyo, mdogo wake ambaye pia ni albino, hajapatikana tangu alipokuwa na umri wa miaka saba. “Kutokana na uhusiano kati ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na Wanasiasa mimi hukaa mbali iwezekanavyo na mikutano ya kampeni za kisiasa,” Bi Manobi alisema. Watu wenye vikwazo katika uhamaji walisema hawaoni ni salama kuhudhuria mikutano ya kampeni ya Siasa kwakuwa hawataweza kujiepusha kwa urahisi endapo kukawa na hali ya vurugu. Walisema hilo huwazuia wao kwenda kukutana / kusikia / kuona Wagombea ili kuwawezesha kufanya uchaguzi wa nani wa kumpigia kura.
Changamoto za ubaguzi hasa kwa jamii kuhusu watu wenye Ulemavu na uwezo wao wa kuwa viongozi pia zimeendelea kuwa kikwazo wanapofikia kuteuliwa kama wagombea katika uchaguzi. Bi Lucia Daudi Mwita aligombea katika Uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita. “Pamoja na kwamba sikuweza kushinda nilikuwa na Uwezo. Jumuiya ilishtushwa kuona mimi kama mwanamke, na mwanamke mwenye ulemavu (amepoteza mkono wake wa kushoto) nilisimama na kuzungumza mbele ya jamii,” alisema Bi Mwita.
Kwa kuhitimisha, mpango kazi wa kuendesha mafunzo uliandaliwa na Viongozi wa vyama vya watu wenye ulemavu, Tanzania ambapo hili litakuwa ni jukumu lao katika wilaya zao kuwafikia watu wengine wenye Ulemavu na kuunga mkono wao kushiriki katika mchakato wa uchaguzi Kidemokrasia na.