UANDIKISHAJI WA WATU WENYE ULEMAVU WENYE SIFA ZA KUAJIRIWA KATIKA KANZI DATA YA CCBRT
Comprehensive Community Based Rehabilitation in Tanzania (CCBRT) ni asasi isiyokuwa ya kiserikali iliyoanzishwa mwaka 1994. Lengo kuu la CCBRT ni kuboresha maisha ya watu wenye Ulemavu kwa kuwapatia huduma za utengamao (rehabilitation services) na kuwawezesha kupata haki zao za msingi na kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo katika jamii.
Hivyo basi CCBRT kupitia kitengo chake cha Ushawishi na Utetezi kinapenda kuwatangazia asasi za watu wenye ulemavu kwamba kimeanzisha dawati la kuwatafutia kazi watu wenye ulemavu wasio na ajira.
Hivyo tunachukua nafasi hii kuwajulisha na kuwahamasisha watu wenye ulemavu waliohitimu kwenye vyuo vikuu na vya kawaida na wenye shahada /stashahada mbalimbali na ambao hawajapata ajira, wajiandikishe kwenye Kanzi data ya CCBRT (data base) kwa lengo la kuwatafutia ajira kwenye Makampuni na mashirika yatakayopenda kufanya kazi na watu wenye ulemavu. Tafadhali, mara usomapo tangazo hili, mjulishe na mwenzio
Waombaji watume CV zao kupitia barua pepe hii:- emmi.kitali@ccbrt.or.tz .
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Emmi Kitali wa CCBRT,
Kitengo cha Ushawishi na Utetezi (Advocacy Unit)
Simu: 0764 645268/0716253674
KARIBUNI!!!