31
Mechi
Warsha ya kukusanya maoni juu ya uandikaji wa Ripoti ya Utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu Wenye Ulemavu, Tanzania
Warsha ya kukusanya maoni kutoka kwa wadau juu ya uwandika wa ripoti mbadala juu ya Utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu Wenye Ulemavu nchini Tanzania, toka kusainiwa na nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania juu ya utekelezaji wa yaliyomo kwenye mkatababa huo mnamo mwaka 2009.
Warsha hio iliyofanyika Tarehe 27/03/2015 ilifanikisha kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali kutoka katika asasi za watu wenye ulemavu na pia wadau waliowakirisha Serikali ambapo mara tu baada ya kumalizika kwa uandikaji wa ripoti hio, itatumwa makao makuu ya Umoja wa mataifa, Geneva, Switzerland.