WARSHA YA KUJADILI KATIBA INAYOPENDEKEZWA NA MASUALA YA WATU WENYE ULEMAVU
Tarehe 26 mwezi Februari 2015 SHIVYAWATA kwa kushirikiana na HANDICAP INTERNATIONAL iliendesha warsha kwa Watu Wenye Ulemavu (WWU) ili kujadili mahitaji ya masuala ya WWU katika katiba mpya.
Mambo kadhaa yalijadiliwa kama;
Masuala yaliojadiliwa katika bunge la Katiba.
Ni yapi yalikuwa mahitaji ya watu wenye ulemavu?
Ni yapi yaliyoingizwa katika katiba.
Nini kifanyike kama katiba itapita au itakataliwa.
Jumla ya washiriki waliohudhuria ni 70 kutoka katika vyama vya watu wenye ulemavu (DPOs) na
asasi za watu wenye ulemavu (PDOs).