19
Februari
MTOTO ALBINO ALIYEKUWA ANASAKWA NA POLISI MKOANI GEITA APATIKANA AKIWA KAFUKIWA HUKU HANA MIKONO NA MIGUU
( Tunaomba radhi kwa picha hii )
Mwili wa mtoto wa mwaka mmoja mwenye ulemavu wa ngozi John Bahati aliyeporwa mikononi mwa mama yake juzi Mkoani Geita, umekutwa jana jioni ukiwa umekatwa miguu na mikono yote na kufukiwa ardhini kwenye hifadhi ya msitu wa Biharamulo, Wilayani Chato.
Pamoja na kuoneka kuwa matukio haya yanazidi kuongezeka nini kifanyike au hakijafanyika kwa usahihi na sisi kama watanzania pamoja na Serikali yetu ?
Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Joseph Konyo katika picha hapo juu amethibitisha tukio hilo kutokea.
Mungu amlaze mahali pema peponi mtoto Yohana Bahati, Amina.
There are 2 comments