SHIVYAWATA imeendesha mafunzo kwa Watu wenye Ulemavu katika mikoa ya Arusha na Lindi
SHIVYAWATA kwa kushirikiana na Handicap International (H.I) kwenye mradi wa From Rights to Inclusion (Kutoka Haki hadi Ujumuishaji ) wiki iliyopita imeendesha mafunzo kwa Watu wenye Ulemavu katika mikoa ya Arusha na Lindi.
Mbunge wa mkoa wa Lindi Bw. Salum Baruani, ambaye pia ana ulemavu wa ngozi (Albinism) pamoja na Afisa Elimu Maalum mkoa wa Lindi Bw. Hassan Nungu na Watu wenye ulemavu 22 walishiriki katika mafunzo.
Mafunzo hayo yalihusu zaidi maeneo yafutayo;
- Maana ya Ulemavu.
- Masuala ya Jinsia na Ulemavu.
- Mbinu za ushawishi na utetezi kwa kutumia sheria za Tanzania na mkataba wa kimataifa wa Watu wenye ulemavu (UNCRPD).
- Maana ya Uongozi na Sifa za Uongozi.
Picha ya Kwanza: Afisa Elimu Maalum mkoa wa Lindi Bw. Hassan Nungu akiwasirisha mada na pembe yake ni Mbunge wa mkoa wa Lindi Bw. Salum Baruani
Picha ya Pili: Baadhi ya Watu wenye ulemavu walioshiriki mafunzo
Picha ya Tatu: Majadiliano yakiendelea katika moja ya vikundi baada ya Mafunzo
Picha ya Nne: Majadiliano yakiendelea katika moja ya vikundi baada ya Mafunzo