22
Januari
SHIVYAWATA yapata alama zaidi ya 80% katika Tathmini iliyoendeshwa na MyRight Sweden
MyRight Sweden mnamo tarehe 14 na 15 mwezi huu Januari waliendesha warsha ya tathmini kwa Shirikisho la Vyama Vya Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA). Warsha hio ililenga zaidi vipengele vilivyoanishwa hapo chini kufanya Tathmini kwa SHIVYAWATA kama Shirikisho, ambapo tathmini ilijumuisha Uongozi, Wadau kutoka vyama vya SHIVYAWATA (Disabled People’s Organisations) na Wafanyakazi ambapo SHIVYAWATA kiujumla ilipata alama zilizozidi 80%.
Vipengele ambavyo tathmini ilijikita zaidi ni kama ifuatavyo
- Tunu na Utambulisho wa Shirikisho
- Uundaji wa dira na dhima ya SHIVYAWATA
- Uundaji wa mikakati muhimu katika uhusiano na dira
- Muundo na Mpangilio wa shughuli wa SHIVYAWATA
- Mgawanyo wa kazi na majukumu
- Matumizi ya sheria za kidemokrasia
- Utekelezaji wa shughuli za SHIVYAWATA
- Mipango kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli
- Kufuatilia na kujifunza kutokana kazi zilizofanyika
- Maudhui ya shughuli yanahusiana na dira
- Njia za ufanyaji kazi zinahusiana na dira
- Ujuzi wa haki kuhusiana na shughuli zinazofanyika
- Taaluma na uzoefu wa wafanyakazi
- Uwezo wa usimamizi
- Muundo wa masuala ya fedha na utawala
- Utawala wa rasilimali fedha
- Makundi yanayolengwa na SHIVYAWATA
- Uungwaji mkono na kukubaliwa pamoja na walengwa
- Maelewano na walengwa wa SHIVYAWATA
- Mazingira ya kazi
- Uhalali wa shughuli zinazoendeshwa na SHIVYAWATA
- Ushiriki katika mtandao na mashirika mengine