26
Juni
SHIVYAWATA IMETIA SAINI UTEKELEZAJI WA MRADI WA UCHAGUZI JUMUISHI NA UMOJA WA MATAIFA KITENGO CHA WANAWAKE
UTANGULIZI: Shirikisho la Vyama Vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania – SHIVYAWATA limetia saini mkataba wa mwaka mmoja na “United Nations (UN) Women” tarehe 20 Mei 2015 kuanza utekelezaji wa mradi wa “Inclusive Election (Uchaguzi Jumuishi) ”. Mradi huu wa Uchaguzi Jumuishi utawezesha Watu Wenye Ulemavu (W.W.U) kushiriki katika siasa na mchakato wa uchaguzi kiujumla Tanzania Bara na Zanzibar. SHIVYAWATA inashirikiana na Umoja wa Walemavu Zanzibar (UWZ) kufanikisha utekelezaji wa mradi Zanzibar.
Malengo ya Mradi: Mradi una malengo makuu matatu kama ifuatavyo;
- Kufanya ushawishi kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Tanzania Bara- NEC na Zanzibar – ZEC juu ya changamoto zinazowakabili W.W.U kushiriki katika mchakato wa uchaguzi na kutoa mapendekezo ya jinsi ya kukabiliana nazo ili kuwezesha ujumuishaji na ushiriki wa W.W.U katika mchakato wa uchaguzi.
- Kuwajengea uwezo W.W.U katika mikoa itayohusishwa na utekelezaji wa mradi juu ya haki na fursa katika mchakato wa kidemokrasia wa uchaguzi kama watangaza nia na wapiga kura.
- Kufanya ushawishi kwa vyombo vya habari juu ya Uongozi kwa W.W.U, Haki za kisiasa na changamoto kwa W.W.U ili kuwapatia nafasi na kutoa taarifa zitakazoshawishi jamii kuondokana na fikra hasi juu ya ushiriki wa W.W.U katika mchakato wa uchaguzi.
Katika Picha: Mkutano wa kuwasilisha mada kuhusu vikwazo kwa W.W.U katika kushiriki uchaguzi na mapendekezo kutoka kwa W.W.U
There are 2 comments