SIKU YA KIMATAIFA YA WATU WENYE ULEMAVU – 3 DESEMBA
2014 Kauli Mbiu · Maendeleo Endelevu: Ahadi ya Teknolojia
~~~~~~Kitaifa itaadhimishwa mkoani Iringa~~~~~~~~~
Mwaka huu Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu italenga jukumu la teknolojia katika:
- Kupunguza athari za maafa na kuongeza muitikio wa dharura
- Kuwezesha mazingira rafiki ya Kazi
- Ujumuishaji endelevu wa malengo ya masuala ya watu wenye ulemavu
Maadhimisho ya kila mwaka ya Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu yalitangazwa na kuzinduliwa mnamo mwaka 1992, kwa tamko la Umoja wa Mataifa katika Mkutano Mkuu – Azimio 47/3. Maadhimisho ya Siku yana lengo la kukuza uelewa wa masuala ya ulemavu na kuhamasisha kuungwa mkono kwa kuthamini utu, haki na ustawi wa watu wenye ulemavu. Pia yanalengo la kuongeza uelewa wa faida zinazoweza kupatikana kutokana na ushirikiano wa watu wenye ulemavu katika kila nyanja ya maisha yakiwemo ya kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiutamaduni.
Tangu mwaka 2009, Idara ya Uchumi na Masuala ya Jamii ya Umoja wa Mataifa, ilianzisha tamasha la filamu kama sehemu ya matukio kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Watu Wenye Ulemavu. The United Nations Enabled Film Festival (UNEFF) pamoja na filamu fupifupi zenye maudhui ya masuala ya Watu Wenye Ulemavu kuhusiana na utambuzi misingi ya muktadha na jumbe zinazo kuza uelewa wa masuala ya ulemavu na zaidi kukuza ushiriki madhubuti wa Watu Wenye Ulemavu katika jamii.