Tathmini ya Utekelezaji wa Mradi wa Haki hadi Ujumuishaji, Tanzania
Tathmini ya utekelezaji wa mradi wa Haki hadi Ujumuishaji nchini Tanzania imefanyika jana Makao Makuu ya SHIVYAWATA Taifa, kwa Viongozi wa vyama vya Watu wenye ulemavu, Wafanyakazi waliohusika katika utekelezaji wa mradi pamoja na Watu wenye ulemavu walionufaika na utekelezaji wa mradi huo.
Mradi wa Haki hadi Ujumuishaji umefanyika katika nchi ya Kenya na Tanzania. Kwa upande wa Tanzania, Mradi wa Haki hadi Ujumuishaji ambao unafikia tamati mwezi Machi mwaka huu, umetekelezwa na SHIVYAWATA kwa ushirikiano na Handicap International kwa kuendesha Mafunzo kwa Viongozi wa Vyama vya Watu wenye Ulemavu pamoja na Watu wenye Ulemavu nchini Tanzania juu ya Maana ya Ulemavu, Sera zinazohusu masuala ya Watu wenye Ulemavu, Sheria zinazohusu masuala ya watu wenye Ulemavu, Mafunzo ya Uongozi, Ujasiriamali, Utetezi na Ushawishi n.k
Mradi wa Haki hadi Ujumuishaji nchini Tanzania, umesaidia kuongeza uelewa wa masuala mbalimbali ya Watu wenye Ulemavu hasa masuala ya Haki, Sheria na Sera zinazohusu masuala ya Watu wenye Ulemavu.
Picha 1: Kikao cha Tathmini kwa Wafanyakazi na Katibu Mkuu juu ya Utekelezaji wa mradi wa Haki hadi Ujumuishaji SHIVYAWATA Makao Makuu
Picha Zingine: Wanachama wa Tanzania Albino Society (TAS) – Kinondoni District