UJUMBE WA MGENI RASMI, MH. WILLIAM LUKUVI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA WATU WENYE ULEMAVU
Maadhimisho ya Siku ya kimataifa ya watu wenye ulemavu Tarehe 03 Disemba Mkoani Iringa katika kiwanja cha Kichangani yafana.
Mh.William Lukuvi ambaye alikuwa mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo alihutubia umati wa watu wakiwemo viongozi wa serikali, wadau kutoka taasis mbalimbali za kijamii, watu wenye/wasio na ulemavu ambao wote kwa pamoja walijumuika kuadhimisha siku hio ambayo kila ifikakapo tarehe 03 Disemba huadhimishwa kitaifa na kimataifa.
Ujumbe wa Mh.William Lukuvi katika maadhimisho hayo ulilenga katika mambo makuu manne kwa kutilia maanani dhima ya siku hio kwa mwaka huu 2014 ambayo ni ;
Maendeleo endelevu: Ahadi ya teknolojia.
Mambo hayo makuu katika ujumbe wa Mgeni Rasmi Mh.William Lukuvi ni kama ifuatavyo;
1.Mikataba yote ya Ujenzi wa miundombinu nchini Tanzania lazima ikidhi mahitaji ya watu wenye ulemavu na pia wasanifu, wahandisi na makandarasi wote wanapaswa kuihakikishia Serikali utekelezaji wa mahitaji ya miundombinu hio.
2. Maendeleo ya teknolojia yawe yanazingatia pia mahitaji ya watu wenye ulemavu mfano mabasi kuwa na milango “automatic” kwa ajili ya watu wenye ulemavu, matumizi ya kompyuta kuzingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu, ujenzi wa maabara kuwa na miundombinu inayozingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu n.k
3. Serikali kupitia mamlaka ya mawasiliano (TCRA) ina hakikisha kunakuwa na wakalimani wa lugha za ishara katika programu za televisheni na mjadala juu ya hili unaendelea ikiwa lengo la serikali ni kuona kwamba kila Televisheni ina ajiri wakalimani wa lugha ya ishara.
4. Wito umetolewa kwa umma wa kuto kubagua watu wenye ulemavu badala yake wanapaswa kuhakikisha kwamba watu wenye ulemavu wanapata haki zote za msingi kwa usawa na wengine katika jamii .