5
Mechi
Warsha ya Mpango kazi wa Taifa juu ya utekelezaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Watu Wenye Ulemavu
Tanzania imekuwa ikifafanua Mpango Kazi wa Taifa juu ya Utekelezaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Watu Wenye Ulemavu, baada ya kuridhiwa kwake mwaka 2009.
Ufafanuzi huo umefanyika katika Warsha iliyoendeshwa kwa siku mbili nakushirikisha wawakilishi kutoka Wizara mbalimbali na mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali.
Lengo la warsha lilikuwa kuuelewa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Watu Wenye Ulemavu na kupanga juu ya utekelezaji wake kitaifa na kisekta pia.
Warsha ya Mpango kazi wa Taifa juu ya utekelezaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Watu Wenye Ulemavu ilipangwa na kufanikishwa na SHIVYAWATA , Handicap International na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ( MOHSW ).